• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 2017 wa Baraza la ngazi ya juu la maendeleo la China waweka mkazo katika kukuza mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa

    (GMT+08:00) 2017-03-20 19:14:02

    Mkutano wa 2017 wa Baraza la ngazi ya juu la maendeleo la China unaoandaliwa na Kituo cha utafiti wa maendeleo cha Baraza la Serikali la China unaofanyika mjini Beijing, unaweka mkazo katika kuhimiza mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa.

    Katika ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika jana, naibu waziri mkuu wa China Bw. Zhang Gaoli alisema, inapaswa kusukuma mbele kwa nguvu mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa. Anasema:

    "Mwaka huu inapaswa kupunguza uzalishaji wa chuma na chuma cha pua kwa tani milioni 50, kupunguza uzalishaji wa makaa ya mawe kwa zaidi ya tani milioni 150, na kupunguza uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati ya makaa ya mawe kwa zaidi ya kilowati milioni 50. Aidha, inapaswa kushikilia kanuni kwamba nyumba zinajengwa kutumia na wala sio kwa ajili ya vitega uchumi, na kutoa maelekezo kupunguza akiba kubwa kupita kiasi ya nyumba katika miji ya ngazi ya tatu na ya nne nchini China. Mbali na hayo tunatakiwa kuongeza nguvu katika kupunguza kodi."

    Mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. He Lifeng amesema kwenye mkutano huo kuwa, baada ya juhudi za mwaka mmoja, mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa yamepata mafanikio ya awali, ambapo muundo wa uchumi umekuwa ukiboreshwa, matumizi ya fedha yalchangia asilimia 64.6 ya ongezeko la uchumi kwa mwaka jana, na thamani ya sekta ya huduma katika pato la taifa GDP iliongezeka hadi asilimia 51.6. Ofisa mwandamizi wa Benki ya Dunia Bi. Kristalina Georgieva anasema:

    "Hatua hizo za mageuzi zina umuhimu mkubwa katika kuhimiza ongezeko la uchumi na utoaji wa nafasi za ajira, la sivyo hatutaweza kutimiza ahadi zilizotolewa kwa mujibu wa malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa."

    Katika mkutano huo, maofisa wengi wa serikali ya China wamesisitiza kuwa, watahimiza muundo wa utoaji wa bidhaa kuendana na mahitaji, na kuzidi kuharakisha hatua za kuboresha utoaji wa huduma za umma, miundo mbinu, uvumbuzi na maendeleo na mazingira ya maliasili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako