• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Afghanistan laonesha maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-03-20 19:18:07

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema azimio namba 2344 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Afghanistan lililopitishwa hivi karibuni limeonesha maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

    Azimio hilo lilipitishwa Ijumaa iliyopita, na linaitaka jumuiya ya kimataifa ikusanye maoni ya pamoja ya kuisaidia Afghanistan, kuimarisha ushirikiano wa uchumi wa kikanda kwa kupitia ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja.

    Bibi Hua Chunying amesema, China itashirikiana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, kutekeleza azimio hilo kujiunga na kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kujenga umoja wa maisha ya binadamu wenye amani ya kudumu, usalama, ustawi wa pamoja, na kufungua mlango.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako