• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapendekeza njia ya kukabiliana na msukosuko wa Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-03-20 19:20:56

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amezitaka pande mbalimbali zijizuie na kufanya juhudi kwa pamoja ili kulifanya suala la nyukilia ya Peninsula ya Korea lirudi kwenye njia ya utatuzi wa kisiasa.

    Bw. Wang Yi amesema hayo alipohudhuria mkutano wa mwaka wa Baraza la Maendeleo ya China uliofanyika leo hapa Beijing. Amesema kutokana na pendekezo lililotolewa na China, Korea Kaskazini inatakiwa kusimamisha majaribio ya makombora ya nyukilia, huku Marekani na Korea Kusini nazo zikitakiwa kusimamisha luteka ya kijeshi ya pamoja, ili pande mbalimbali zirudi upya kwenye mazungumzo. Amesema pande mbalimbali zinatakiwa kuunganisha kutimiza lengo la kutokuwepo kwa silaha za nyukilia kwenye Peninsula ya Korea na kuanzisha mfumo wa amani kwenye peninsula hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako