• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) yaingia kambini

    (GMT+08:00) 2017-03-21 08:46:17

    Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimeanza kambi huku kikimkosa mshambuliaji wa kimataifa Thomas Ulimwengu.

    Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas ameeeleza, taarifa ambazo wamezipata toka Sweden ni kwamba Ulimwengu kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo ya AFC Eskilstuna.

    Hivyo sasa kocha wa Taifa Stars, Mayanga atabaki na washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).

    Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25, 2017 kabla ya kuivaa Burundi Machi 28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati huu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako