• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuelekea Kombe la Dunia 2018: Vinara Brazil ugenini na Uruguay

    (GMT+08:00) 2017-03-21 08:49:36

    Mechi za nchi za kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa Shirikisho lao CONMEBOL kusaka nchi 4 zitakazotinga moja kwa moja kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018 zitaendelea Alhamisi wiki hii.

    Baada ya Mechi 12 kwa kila Timu, Brazil ndio wanaongoza wakiwa na Pointi 27 wakifuata Uruguay wenye 23, Ecuador wana 20, Chile 20 na Argentina 19.

    Kwenye Mechi za Wiki hii, mpambano mkali uko huko Montevideo wakati Wenyeji Uruguay wakikwaana na Brazil.

    Mechi nyingine kali ni ile itakayochezwa Buenos Aires kati ya Argentina na Chile. Na nyingine ni kati ya Colombia na Bolivia, Paraguay na Ecuador huku Venezuela wakiivaa Peru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako