• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yamfungia refa kutojihusisha na soka maisha

    (GMT+08:00) 2017-03-21 09:07:13

    Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA jana limetangaza maamuzi kwa refa Joseph Lamptey aliyechezesha mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi kati ya Afrika Kusini dhidi ya Senegal.

    Refa huyo alichezesha mechi hiyo November 12 mwaka jana mechi iliyomalizika kwa Afrika Kusini kupata ushindi wa goli 2-1, Lamptey amefungiwa na FIFA katika ngazi ya kitaifa na kimataifa anatajwa kuhusika na upangaji wa matokeo kwa kufanya maamuzi yake kinyume na sheria wakati wa mchezo huo.

    Kutokana na makosa hayo, amefungiwa maisha kujihusisha na soka yaani kuanzia urefa hadi uongozi wa aina yoyote ule wa soka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako