• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la umeme la China laimarisha ujenzi wake kwa kulinganisha mahitaji ya nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2017-03-21 18:00:47

    Shirika la nishati ya umeme la China linaloshughulikia sekta ya nishati ya umeme, miundo mbinu, maliasili ya maji na mazingira ni moja kati ya kampuni zinazoshika nafasi 500 za mwanzo duniani. Kampuni hiyo imewekeza katika nchi 102 duniani, na kushika nafasi ya kwanza katika sekta ya ujenzi wa nishati ya umeme duniani mwaka 2016. Mwezi Machi, ujenzi wa makao makuu ya kampuni hiyo katika eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika umemalizika, hali inayoonesha kuwa kampuni hiyo itaimarisha ujenzi wake kwa kulingana na mahitaji ya nchi za Afrika.

    Naibu meneja mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Wang Bin alimwambia mwandishi wa habari wa Radio China Kimataifa akisema: "Kampuni ya ujenzi wa nishati ya umeme ya China ikiwa kampuni ya serikali kuu imeweka mipango halisi ya dunia nzima kwa kufuata mikakati ya taifa. Kampuni yetu imeanzisha ofisi sita za makao makuu duniani katika miaka zaidi ya 30 iliyopita, na imepata maendeleo ya kuwanufaisha watu wa sehemu hizo."

    Bw. Wang Bin amesema, makao makuu ya kampuni hiyo yaliyozinduliwa tarehe 8 Machi Nairobi, a Kenya yanashughulikia mambo ya nchi 26 zilizoko mashariki na kusini mwa Afrika zikiwemo Kenya, Ethiopia, Uganda, Tanzania, Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini.

    Ameeleza kuwa, kampuni hiyo inashughulikia mambo ya nishati ya umeme, ujenzi wa miundo mbinu pamoja na maliasili ya maji na mazingira katika nchi hizo za Afrika. Anasema:

    "Kampuni yetu itafanya ujenzi kwa kufuata mahitaji ya nchi hizo za Afrika. Itahamishia teknolojia, huduma pamoja na fedha barani Afrika, hali ambayo itachangia maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi hizo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako