• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasisitiza Korea Kaskazini itekeleze kikamilifu azimio la Baraza la Usalama

    (GMT+08:00) 2017-03-21 19:34:56

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameisisitiza Korea Kaskazini itekeleze azimio la Baraza la Usalama la Umoja huo kwa pande zote na kuepuka vitendo zaidi vya uchokozi.

    Hayo yamesemwa na msemaji wa katibu mkuu huyo Farhan Haq kufuatia Korea Kaskazini kufanya jaribio la kuwasha injini ya roketi itakayotumika kurusha makombora. Amesema, Bw. Guterres anafuatilia kwa karibu majaribio mbalimbali ya kurusha makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini, na ameitaka Korea Kaskazini itekeleze azimio la Baraza la Usalama na kutekeleza jukumu lake la kimataifa kwa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako