• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Israel

    (GMT+08:00) 2017-03-21 20:17:02

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu, ambapo wametangaza kuanzisha uhusiano wa wenzi wa pande zote.

    Rais Xi amesema kuwa pande hizo mbili zitaimarisha mawasiliano ya kisiasa, kukuza maelewano na uaminifu, na kuhimiza miradi muhimu ya ushirikiano kwa hatua madhubuti kwa kufuata mpango wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Bw. Netanyahu amesema, Israel inapenda kujiunga na ushirikiano wa ujenzi wa miundo mbinu kwa kufuata mpango huo, na inatumai kuwa China itachangia zaidi katika mambo ya Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako