• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kampuni za usambazi habari Tanzania kufanya mabadiliko ya kiutendaji

    (GMT+08:00) 2017-03-21 21:03:10

    Kampuni za usambazi habari nchini Tanzania Mwananchi Communications Ltd (MCL) wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti inafanya mabadiliko ya kiutendaji ili kuendana na mazingira ya soko na uchumi wa hivi sasa.

    Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai amesema hay oleo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mwananchi jijini Dar es Salaam.

    Amesema kampuni inafanya mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutendaji ili kuwafikishia wateja habari za uhakika zaidi na kwa haraka kupitia mfumo wa (digitali).

    Amesema kuwa kampuni hiyo pia inafanya mabadiliko makubwa katika maeneo ya kubana matumizi katika maeneo mbalimbali ya kiuendeshaji, kusimamisha ajira zilizokuwa zimeidhinishwa kwa mujibu wa bajeti ya kampuni ya mwaka 2016/2017 na kupunguza matumizi katika bajeti ya mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi.

    Maeneo mengine yenye mabadiliko ni kupunguza safari za mafunzo na kikazi na kusitisha kuongeza mishahara kwa mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako