• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Watanzania watakiwa kununua bidhaa kutoka nchi mbalimbali

    (GMT+08:00) 2017-03-21 21:04:29

    Mwenyekiti wa jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Tanzania Johnson Minja amewashauri wafanyabiashara kununua bidhaa kutoka nchi mbalimbali ili kuepuka kuingiza nchini bidhaa zinazofanana.

    Akizungumza na wawakilishi wa kampuni kumi kutoka nchini Mauritius waliokuja kuangalia fursa za kibiashara nchini Minja amesema bidhaa zinazouzwa katika maeneo mbalimbali zinafanana kutokana na bidhaa hizo kutoka katika nchi moja jambo ambalo halitakiwi.

    Kwa upande wake afisa biashara za nje kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini TANTRADE Steven Kobelo amesema bidhaa ambazo watanzania wanaweza kupeleka Mauritius ni vyakula pamoja na malighali ya kutengenezea nguo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako