• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Bei ya unga wa mahindi yapanda

    (GMT+08:00) 2017-03-21 21:04:48

    Bei ya unga wa mahindi nchini Kenya imeongezeka hadi Sh130 kwa pakiti ya kilo mbili.

    Haya yamejiri wakati ambapo wenye viwanda vya kusaga mahindi wameonya kuwa bei hiyo huenda ikaendelea kuongezeka katika siku zijazo kwa sababu ya upungufu wa mahindi katika soko.

    Kutokana na kupanda kwa gharama za chakula maji nchini Kenya,mfumuko mwezi Januari uliongezeka hadi asilimia 9.04.Hii imesababishwa na kiangazi cha muda mrefu nchini kote.

    Mwezi uliopita bei ya unga wa mahindi ilishuka kutoka bei ya wastani ya Sh128 kwa pakiti ya kilo mbili hadi Sh123 huku wenye viwanda vya kusaga mahindi wakisema walilazimika kushusha bei zao kwa sababu kampuni ya Jamii Unga ilipunguza bei,na hivyo kuwalazimu wengine kufanya hivyo ili kuleta ushindani katika soko.

    Hivi sasa unga wa mahindi wa chapa ya Jogoo unauzwa kwa Sh130 kutoka Sh126 wiki iliyopita,Ndovu Sh130 kutoka Sh123,Soko Sh131 kutoka Sh123 na Kifaru Sh129 kutoka Sh123.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako