• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TFF yakanusha taarifa za mechi kati ya Taifa Stars na Chipolopoolo ya Zambia

    (GMT+08:00) 2017-03-22 08:43:51

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limekanusha taarifa zilizotolewa na Shirikisho la Soka nchini Zambia(FAZ) juu ya uwepo wa mechi ya kirafiki iliyopaswa kupigwa machi 24 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema jana, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema hawajapata taarifa yoyote ya kuthibitishwa kuwepo kwa mchezo wa kirafiki baina ya nchini hizo ambao umedaiwa kupigwa machi 24 na 26 katika uwanja wa Taifa.

    Amesema ni kweli TFF iliomba kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Chipolopolo lakini kutokana na shirikisho hilo kuchelewa kujibu maombi yao waliamua kuomba mechi nyingine kutoka kwa nchi nyingine ambazo tayari ratiba yao inatambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika.

    Amedai TFF iliamua kuomba mchezo mwingine wa kirafiki kwa Burundi na Botswana ambayo itapigwa Machi 25 na 28 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako