• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TP Mazembe yamtimua kocha baada ya kuvurunda Ligi ya Mabingwa

    (GMT+08:00) 2017-03-22 08:44:54

    Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo (DRC) imeachana na kocha Mfaransa, Thierry Froger baada ya kutolewa katika hatua hatua ya 32 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika na CAPS United ya Zimbabwe kwa mabao ya ugenini, ikitoa sare ya 1-1 Lubumbashi na 0-0 Harare.

    Mazembe imeangukia katika kapu la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na itamenyana na JS Kabylie ya Algeria. Froger alijiunga na Mazembe Februari 15, siku chache kabla ya kumenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mechi ya Super Cup ya CAF, akichukua nafasi ya Mfaransa mwenzake, Hubert Velud aliyeondoka mwishoni mwa mwaka jana kuhamia Etoile du Sahel ya Tunisia.

    Mechi za kwanza zinatarajiwa kucheza wikiendi ya Aprili 7 hadi 9 na marudiano yanatarajiwa kuwa wikiendi ya Aprili 14 hadi 16, mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako