• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya Lisbon Half Marathon, Kenya yaelemewa

    (GMT+08:00) 2017-03-22 08:45:12

    Wakenya Vivian Cheruiyot na James Wangari Mwangi walizidiwa kasi ya kumaliza mbio na kumaliza katika nafasi za pili za Lisbon Half Marathon nchini Ureno.

    Bingwa wa Olimpiki mita 5,000 mwaka 2016, Cheruiyot, ambaye anafahamika kwa jina la utani kama "Pocket Rocket" alilemewa kwa sekunde moja na bingwa wa marathon duniani Mare Dibaba.

    Muethiopia Dibaba alimaliza mbio hizo kwa saa 1:09:43 naye Cheruiyot alikamilisha umbali huo wa kilomita 21 kwa saa 1:09:44. Mshindi wa Houston Half Marathon mwaka 2016 Mary Wacera kutoka Kenya alishikilia nafasi ya tatu kwa saa 1:09:53.

    Kwa upande wa wanaume, James Wangari Mwangi aliibuka mshindi wa pili baada ya kutumia saa 1:00:11 nyuma ya Jake Thomas Robertson wa New Zealand aliyekuwa mshindi wa kwanza kwa kutumia saa 1:00:01 na Edwin Kibet Koech kuwa mshindi wa tatu baada ya kutumia saa 1:00:45

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako