• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkufunzi wa zamani Liverpool Ronnie Moran afariki dunia

    (GMT+08:00) 2017-03-23 08:45:19
    Nahodha na mkufunzi wa zamani Liverpool Ronnie Moran amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83.Moran alichezea klabu hiyo mechi 379 kati ya 1952 na 1966.

    Alikuwa mfanyakazi aliyeitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi alipostaafu 1999. Alijiunga na benchi la wakufunzi Liverpool mwaka 1966 na mara mbili alihudumu kama meneja wa muda, baada ya Kenny Dalglish kujiuzulu 1991 na Graeme Souness alipofanyiwa upasuaji wa moyo 1992.

    Mwanawe wa kiume amethibitisha kwamba alifariki mapema Jumatatu baada ya kuugua kwa muda mfupi. Alihudumu chini ya mameneja tisa tofauti alipokuwa benchi la kiufundi.

    Aidha aliwaongoza Liverpool fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley mwaka 1992 akiwa meneja wa muda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako