• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester City na Manchester United kukipiga Marekani

    (GMT+08:00) 2017-03-23 08:46:02

    Derby ya mahasimu wa Jiji la Manchester, Manchester City na Manchester United, itahamia nchini Marekani, kwa mchezo wa kirafiki kupigwa Julai 20 mwaka huu. Mchezo huo, wa kwanza wa kihistoria kuwahi kupigwa nje ya Uingereza, bado haujapangiwa uwanja utakaofanyika, lakini upo kwenye ratiba ya michezo ya mashindano ya International Champions Cup.

    Mahasimu hao, walikosa kuchuana nje ya Uingereza mwaka uliopita, kwa mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu hapa Beijing China kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.

    Manchester City pia itakipiga na vigogo wengine wa ligi ya Uingereza, Tottenham Hotspurs, Mjini Nashville Julai 29, kabla ya kukutana na Real Madrid Jijini Los Angeles Julai 26 .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako