• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usain Bolt awaalika David Rudisha na Mo Farah kushiriki shindano lake la mwisho

    (GMT+08:00) 2017-03-23 08:46:54

    Mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani Usain Bolt amemwalika mfalme wa mbio za mita 800 duniani David Rudisha na yule wa mita 5,000 na 10,000 Mo Farah, kushiriki kwenye shindano lake la mwisho la kumuaga anapojiandaa kustaafu riadha mwaka huu.

    Rudisha anayeshiklilia rekodi ya dunia katika mbio hizo na Mwingereza Mo Farah ni miongoni mwa wanaridha nyota walioalikwa kushiriki kwenye mbio za Racers Track Club Grand Prix mwezi ujao Aprili 10, litakalokuwa shindano lake la mwisho Bolt kisha kustaafu riadha akiwa na umri wa miaka 30.

    kuhusu shindano hilo lenye kauli mbiu ya 'Salute to a Legend'. litaandaliwa nyumbani kwao katika jiji kuu Kingston, Jamaica ambapo Bolt atakanyaga lami mbele ya maelefu ya wananchi wenzake ambao ni mashabiki wake wakubwa.

    Katika muda wake wa riadha, Bolt ameshinda jumla ya medali nane za dhahabu za Olimpiki katika vitengo vya mita 100, 200, 400.

    Aidha ni mwanariadha wa kwanza kushikilia rekodi ya dunia kwenye mita 100 na mita 200. Pia ni bingwa mara 11 wa shindano la dunia (World Championships) katika vitengo hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako