• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa China atoa mwito wa suala la Syria kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2017-03-23 09:17:30

    Mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia suala la Syria Bw. Xie Xiaoyan jana huko Geneva alifafanua msimamo wa China juu ya suala la Syria, na kutoa mwito wa suala hilo kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

    Bw. Xie amesema pande mbalimbali zinatakiwa kusimamisha mapambano, kuweka mazingira ya mchakato wa kisiasa, na kufanya mazungumzo ya amani.

    Ameongeza kuwa suala la Syria lina utatanishi na linahusu mambo mengi yakiwemo mchakato wa kisiasa, usitishaji vita, misaada ya kibinadamu, na mapambano dhidi ya ugaidi.

    Serikali ya Syria na wapinzani wanatakiwa kufanya mawasiliano na mazungumzo ili kutafuta ufumbuzi wa kisiasa unaoendana na maslahi ya muda mrefu ya watu wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako