• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yawarudisha wakimbizi zaidi ya 57,000 wa Somalia walioko Kenya

    (GMT+08:00) 2017-03-23 09:42:14

    Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema limewarejesha nyumbani wakimbizi zaidi ya elfu 57 wa Somalia walioko Kenya tangu mwezi Desemba mwaka 2014.

    Kamishna mwandamizi wa UNHCR amesema katika wiki mbili zilizopita wakimbizi karibu elfu 4 wameondoka Nairobi na kurejea Somalia.

    UNCHR imesema mwaka huu wakimbizi wengine 17,359 kutoka kambi ya Dadaab iliyoko kaskazini mashariki mwa Kenya wamerejea nyumbani.

    Msafara wa magari kutoka Dadaab hadi Dhobley ziliandaliwa kwa ajili ya wakimbizi hao kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi kila wiki. Zaidi ya hayo, safari ya ndege kwenda Mogadishu imerejeshwa tangu tarehe 27 mwezi uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako