• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yasema kuwa, mipaka kuhusu umiliki wa hisa wa wawekezaji wa nchi za nje itaondolewa katika baadhi ya sekta

    (GMT+08:00) 2017-03-23 17:10:22

    Wizara ya biashara ya China leo imeandaa mkutano na waandishi wa habari kujibu maswali ya sekta ya biashara yanayofuatiliwa zaidi hivi karibuni. Msemaji wa wizara hiyo Bw. Sun Jiwen amesema, wizara hiyo inashirikiana na idara zinazohusika kufanya marekebisho kuhusu Orodha ya kuelekeza kampuni za nchi za nje kuwekeza nchini China iliyochapishwa mwaka 2015, ambapo mipaka kuhusu umiliki wa hisa za wawekezaji wa nchi za nje itafutwa katika baadhi ya sekta.

    Bw. Sun Jiwen akijibu swali kuhusu madai ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa wawekezaji wengi wa nchi za nje wanatakiwa kuanzisha kampuni za ubia nchini China na kuuza teknolojia zao, na hatua hiyo imekiuka kanuni zinazohusika za Shirika la biashara duniani WTO, amesema kwamba kwa mujibu wa sheria na kanuni za uwekezaji wa kampuni za nchi za nje zinazotekelezwa nchini China, kiasi kikubwa cha sekta ziko wazi kwa wawekezaji wan chi za nje, isipokuwa sekta chache zinazohusu mambo nyeti. Hivi sasa China inafanya marekebisho kuhusu orodha hiyo na kuzidi kupunguza idadi ya sekta zinazoweka mipaka kuhusu umiliki wa hisa wa wawekezaji wa nchi za nje. Bw. Sun anasema:

    "Hivi sasa Wizara ya biashara inashirikiana na idara zinazohusika kufanya marekebisho kuhusu Orodha ya kuelekeza kampuni za nchi za nje kuwekeza nchini China iliyochapishwa mwaka 2015, na kuzidi kupunguza idadi ya sekta zinazowekewa mipaka kuhusu kiasi cha umiliki wa hisa wa wawekezaji wa nchi za nje."

    Msemaji huyo pia amesisitiza kuwa, kwa kufuata sheria zinazotekelezwa hivi sasa nchini China, hakuna madai kwa wawekezaji wa nchi za nje kuuza teknolojia. Kinyume chake, serikali ya China inazihimiza kampuni za China kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa teknolojia ya kampuni za nchi za nje. Na masharti halisi ya ushirikiano yanayohusishwa katika mazungumzo kati ya wafanyabiashara wa nchi za nje na China ni kitendo cha kawaida katika soko, hakipaswi kuchukuliwa kama ni hatua ya kuwalazimisha wafanyabiashara wa nchi za nje kuuza teknolojia.

    Akizungumzia kitendo cha nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na Marekani kutumia "nchi mbadala" isio China kuhesabu gharama za utengenezaji inapofanya uchunguzi dhidi ya bidhaa za China zinazoshukiwa kuuzwa kwa bei nafuu kupita kiasi katika masoko, Bw. Sun Jiwen anasema:

    "Hivi karibuni China itautaka mkutano wa WTO unaoshughulikia utatuzi wa migogoro kufikiria tena dai la China, na kikundi cha wataalamu kitaundwa. China ina imani kubwa kuwa WTO itatoa hukumu kwa haki, pia imeihimiza Ulaya itekeleza kwa hatua halisi jukumu la WTO, na kubadilisha kitendo chenye lengo lisilo na maana la kutumia "nchi mbadala" isiyo China kuhesabu gharama za utengenezaji inapofanya uchunguzi dhidi ya bidhaa za China zinazoshukiwa kuuzwa kwa bei nafuu kupita kiasi katika masoko."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako