• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakaazi wa Kibera mjini Naiorbi wapokea msaada kutoka kwa wachina

    (GMT+08:00) 2017-03-23 18:15:36

    Wakaazi wa Kibera mjini Nairobi wamepokea msaada kutoka kwa Sino Africa Firefly Charity ulioanzishwa hivi karibuni na daktari mmoja wa China nchini humo.

    Msaada huo ulijumuisha unga na sodo kwa wanawake kama anavyoripoti Serah Nyakaru kutoka Nairobi.

    Makati wa Ni wakaazi wa kibera wakati wa hafla ya kupokea msaada huo kutoka kwa jamii ya Wachina.

    Baadhi ya misaada ni pamoja na unga na sodo.

    Kibera ni mojawepo wa mitaa ya mabada mjini Nairobi ambako kulingana na benki ya dunia watu wengi wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku.

    Wanalionufaika na msaada wa leo kama vile mama Evelyn Adega wanasema umekuja kwa wakati unaofaa.

    Ikiwa na jina Sino Africa Firefly Charity, msaada huu wa kibera ni maalum na wa aina yake kwa wakaazi wa Kibera.

    Mwanzilishi wake Daktari Lei Wang anawaalika wachina kutembelea moja kwa moja wakaazi wa hapa na kutoa misaada wao wenyewe.

    Kwa kufanya hivyo wanaweza kujumuika na wenyeji na pia kujionea hali ya maisha yao ya kila siku huku wakitoa mchango wao kama sehemu ya wajibu wa wachina kwa jamii nchini Kenya.

    Daktari Lei Wang alikuja Kenya hususan kutoa huduma za matibabu kwa watu walio na mapato ya chini.

    Lakini baadaye akaguzwa na hali ya umaskini katika baadhi na maeneo na hivyo kuanzisha mpango wa utoaji msaada.

    Anaona kwamba msaada huu licha ya kuwa ni mdogo lakini utafungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa China na Kenya.

    "Leo anayetoa msaada wake ni mojawepo wa kampuni ya China kwa jina GTT na inatoa msaada wake kwa mara ya nne chini ya mpango wetu wa Sino Africa Firefly Charity. Katika siku za baadaye tutaendelea kufanya kazi kwa bidii kwa watu wanaoishi katika mtaa wa kibera. Ushirikiako wa China na Afrika una historia ndefu. Lengo la Sino Africa Firefly Charity ni kukuza ushirikiano wa watu kwa watu kati ya Wachina na Wakenya . Tunaamini kwamba tukiongozwa na mkakati wa Njia moja na Ukanda mmoja tukakuwa na mafanikio mapya nchini Kenya"

    Nchini Kenya kama vile nchi nyingi barani Afrika kuna ongezeko la uwekezaji kwenye sekta mbali m bali.

    Kwa sasa Kenya ina zaidi ya kampuni 400 za wawekezaji wa China hali ambayo imechangia upatikanaji wa ajira kwa vijana na ushuru kwa serikali.

    Lakini pia kampuni hizo zimechangia pakubwa kwenye utoaji wa huduma kwa jamii kama vile kampuni ya GTT ambayo leo imetoa msaada kwa wakaazi wa Kibera.

    Bwana Kunhu Yang ni mkurungezi wa kampuni hiyo nchini Kenya.

    ""

    Katika siku za nyuma pia kampuni nyingine za china nchini Kenya kwa kushirikiana na ubalozi zimetoa misaada ya chakula kwa waanga wa ukame katika maeneo mbalimbali.

    Hata hivyo, wakifahamu vyema kwamba msaada sio suluhu la kudumu kwa matatizo kama vile uhaba wa chakula, wachina wengi kupitia kwa makampuni yao wanasaidia jamii kuwa na miradi endelevu ya kujipatia sio tu chakula lakini pia na mapato.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako