• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Treni kwenye reli ya kisasa nchini Kenya kutumia umeme baada ya miaka minne

    (GMT+08:00) 2017-03-23 18:20:41

    Treni kwenye reli ya kisasa nchini Kenya inayojengwa na kampuni ya China, itaanza kutumia umeme baada ya miaka minne.

    Waziri wa uchukuzi James Macharia, amesema kupandishwa kwa hadhi ya reli hiyo ili ianze kutumia umeme kutagharimu asilimia 15 ya pesa zote zilizotumika kwenye mradi huo hadi sasa.

    Alisema kwenye hatua za mwanzo serikali haikuwa na mpango wa kuweka umeme kwenye reli hiyo kwa sababu Kenya bado haina kawi ya kutegemewa ya kuendesha treni bila kutatika.

    Kwa sasa reli hiyo kutoka Mombasa hadi Nairobi ina urefu wa kilomita 472 na imegharimu shilingi bilioni 328.

    Serikali inatarajia kwamba reli hiyo itasafirisha tani milioni 22 za shehena kila mwaka ikilinganishwa na ile ya sasa inayosafirisha tani milioni 2 tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako