• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Benki za Kenya zalalamika kuhusu sheria ya udhibiti wa riba

    (GMT+08:00) 2017-03-23 18:22:05

    Benki za Kenya zimelalamika kuhusu sheria ya udhibiti wa riba iliyotiwa saini na rais Uhuru Kenyatta mwaka uliopita kwa kusema inaziletea hasara.

    Kwa mujibu wa chama cha wanabenki KBA, utafiti uliofanywa na chama hicho umeonyesha kuwa asilimia 47 ya wateja wao hawajafurahishwa na sheria hiyo. Chama hicho kinadai kuwa benki zimelazimika kuweka tahadhari zaidi kabla ya kuwapa mikopo. Afisa mkuu mtendaji wa KBA Habil Olaka amesema kiwango cha pesa za mikopo kwa wateja kimepungua kwa asilimia 10.3. Pesa ambazo wateja wa benki walichukua mikopo zilipungua kutoka shilingi bilioni 630 hadi 520 katika benki zote kwa kipindi cha miezi sita iliyopita. Sheria hiyo iliyoanza kutumika Septemba iliweka kiwangocha juu zaidi cha riba ya mikopo ya benki kuwa asilimia 14.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako