Mkutano wa mwaka 2017 wa Baraza la Asia la Bo'ao umefanyika leo huko Bo'ao, mkoani Hainan, China, na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 1,800.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni "Kukabiliana na utandawazi wa dunia nzima na mustakabali wa biashara huria". Katibu mkuu wa baraza hilo Bw. Zhou Wenzhong amesema, mkutano huo utahusisha mambo yanayohusu "Ukanda Mmoja, Njia Moja", "ongezeko", "mageuzi", na "uchumi wa aina mpya".
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |