• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsenal yasitisha mazungumzo kuhusu mikataba ya Alexis Sanchez na Mesut Ozil

    (GMT+08:00) 2017-03-24 08:34:16
    Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema klabu hiyo imesitisha kwa muda mazungumzo kuhusu mikataba ya Alexis Sanchez na Mesut Ozil hadi mwisho wa msimu. Mikataba ya Sanchez na Ozil katika klabu ya Arsenal inamalizika mwezi juni mwakani na wamekuwa wakisusua kusaini mikataba mipya ya kuendelea kuitumika timu hiyo.

    Arsenal wameshuka hadi nambari sita Ligi ya Premia baada ya kushindwa mechi nne kati ya tano walizocheza karibuni zaidi.

    Kuhusu mustakabali wake, Wenger alisema bila kujali atasalia klabunii kwa muda gani, bado ataendelea kujitolea na kutimiza majukumu yake muda wote atakaokuwa katika klabu hiyo.

    Gunners watarejea uwanjani Ligi ya Premia Jumapili tarehe 2 Aprili watakapokuwa wenyeji wa Manchester City.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako