• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • England yakubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ujerumani

    (GMT+08:00) 2017-03-24 08:34:50

    Timu ya taifa ya England imekubali kichapo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki.

    Bao pekee la ushindi katika mchezo huo liliwekwa kimiani na mshambuliaji Lukas Podolski katika dakika ya 69 ya mchezo kwa shuti kali la umbali wa mita 25 lilomshinda kipa wa England Joe Hart. Mchezo huu wa kirafiki ulikua ni wa mwisho kwa mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Ujerumani Lukas Podolski anayestaafu soka ya kimataifa akiwa na umri wa miaka 31. Mshambuliaji huyu alianza kuichezea timu ya taifa ya wakubwa mwaka 2004 na kufunga jumla ya magoli 49 katika michezo 130.

    Wakati huohuo meneja wa England, Gareth Southgate, amesema amefurahishwa sana na jinsi upande wake ulivyokumbatia mfumo mpya wa mchezo katika mechi hiyo. Southgate alisema ameamua England icheze ikitumia mfumo wa 3-4-3 karibu wiki sita zilizopita. Alitumia mabeki watatu kwa mara ya kwanza tangu kushindwa kwao na Croatia mwaka 2006.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako