• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Uganda hakuna mbabe kwenye mechi ya kirafiki

    (GMT+08:00) 2017-03-24 08:35:06

    Mzaha wa mabeki wa Kenya umeifanya Harambee Stars jana ipokonywe ushindi katika dakika za lala-salama za mechi ya kirafiki dhidi ya Uganda iliyomalizika kwa 1-1 uwanjani Kenyatta mjini Machakos.

    Katika mechi hii ya 11 ya kocha Stanley Okumbi, Michael Olunga aliipa Stars uongozi dakika ya 34 kabla ya Moses Waiswa kuvunja mioyo ya maelfu ya Wakenya waliofika uwanjani baada ya kusawazisha katika dakika ya 87. Licha ya kudumisha rekodi ya kutoshindwa hadi mechi tisa, Okumbi hakufurahishwa na matokeo. Kenya ilipata nafasi nne nzuri katika kipindi cha kwanza.

    Hata hivyo Uganda iliiwekea Kenya shinikizo katika kipindi cha pili. Mawasiliano mabaya katika safu ya ulinzi ya Kenya yalimtunuku Waiswa nafasi nzuri nje ya kisanduku.

    Baada ya kujipima nguvu na Uganda inayoshika nambari 74 duniani, Kenya, ambayo inashikilia nafasi ya 88 duniani, itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Leopards ya DR Congo mnamo Machi 26 uwanjani Kenyatta. Kenya, ambayo inatarajiwa kukaribisha nyota wa Tottenham Hotspur Victor Wanyama dhidi ya DR Congo, inatumia mechi hizi kujipiga msasa kabla ya kuanza safari ya kutafuta tiketi ya kuenda Cameroon mwaka 2019 kwa Kombe la Afrika (AFCON).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako