• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Azama FC yasubiri ripoti ya Kamishna wa michezo baada ya vurugu nchini Swaziland

    (GMT+08:00) 2017-03-24 08:35:38

    Klabu ya Azam FC imesema, wanasubiri ripoti ya Kamishna wa mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows juu ya vurugu zilizotokea katika mchezo huo uliopigwa Machi 19 Uwanja wa Taifa wa Somhlolo, nchini Swaziland

    Afisa habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema, wameamua kumuachia kamishina wa mchezo kila kitu kwani yeye alishuhudia vurugu zote zilizotokea kabla ya mchezo huo.

    Amesema Kamishna aliruhusu wachezaji wa Azam FC kubadilishia nguo ndani ya gari mara baada ya kujiridhisha na hali iliyokuwa ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.

    Maganga amesema, mbali na matukio hayo waliweza kukubali matokeo ya mchezo huo ambao walifungwa mabao 3-0 na kutolewa katika mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako