• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzinduzi wa maonyesho ya tamthilia ya China Mfalme Kima wafanyika Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-03-24 09:14:33

    Wizara ya mawasailiano na habari nchini China ikishirikiana na wizara ya habari sanaa na michezo nchini Tanzania zimezindua rasmi maonyesho ya filamu ya kichina ya kwa jina Mfalme Kima iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

    Filamu hii iliyowekwa tafsiri kwa uongozi wa idhaa ya Radio China kimataifa itaonyeshwa kupitia kwa televisheni ya TBC kote Tanzania na inalenga kuendeleza ushirikiano wa mila na tamaduni za China na Tanzania.

    Filamu ya Mfalme Kima imeigizwa na wachina na kutiwa sauti na watanzania ishara kamili kwamba ushirikiano wa China na Tanzania unazidi kushamiri.

    Waziri wa habari filamu na televisheni wa China Gong Tong aliyeongoza maonyesho haya amevutiwa sana namna filamu za China zinavozidi kuvutia mashabiki wa nchi za Afrika .

    Amesema utafiti unaonyesha kwamba idadi kubwa ya watanzania wanapenda filamu zilizotafsiriwa kwa kiswahili jambo ambalo linaonyesha hatua kubwa iliyopigwa kwenye ushirikiano wa kimila na utamaduni baina ya nchi hizi mbili.

    Kwa mujibu wa utafiti,katika kila kundi la watanzania 140 waliohojiwa kuhusiana na tamthilia za China ,137 wa nufahamu na ni mashabiki.

    Elesante Ole Gabriel katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano sanaa na michezo Tanzania amesema balozi ya China nchini Tanzania inafanya mikakati mengi kuhakikisha nchi hizi mbili zinaendeleza utamaduni na kubuni ajira nchini Tanzania.

    Ametoa mwito wa kwamba lugha ya kiswahili sasa inapaswa kutumika katika filamu za wachina zinazoonyeshwa nchini China ili wachina zaidi wafahamu kiswahili.

    Takwmimu zinaonyesha kwamba watu milioni 8 nchini Tanzania wanatazama filamu za kichina zilizotiwatafsiri ya kiswahili.

    China hutumia teknolojia za kisasa katika kutayarisha filamu kwa ubora wa juu.

    Tanzania sasa inalenga kushirikiana na China katika teknolojia hiyo kwani wamepata fursa ya kusafirisha wadau wa tasnia ya filamu na televisheni China kwa mafunzo.

    Fauka ya hayo Tanzania sasa inalenga kupata soko la Filamu la China ambalo lina watazamaji zaidi ya bilioni moja kama anavoelezea Suzana Mungy mkurugenzi mkuu wa habari katika kituo cha televisheni cha TBC.

    'Filamu za wachina zinapendwa sana ,tamthiliaya Mama dodo ilileta mashabiki wengi sana,sasa tunachohitaji ni wachina kuigiza pamoja na watanzania kwenye filamu moja na pia wachina waje Tanzania kufanya kazi kwenye televisheni kwani wanajua kiswahilia sana'

    Ametoa changamoto ya China na Tanzania kushirikiaana na kuigiza tamthilia kwa kutumia waigizaji wa kichina na watanzania.

    Hii sio tamthilia ya kwanza kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili,tamthilia ya Mama dodo na wakwe zake iliyotiwa sauti na waigizaji wa Kenya ilifungua milango ya mashabiki wengi kutoka Afrika Mashariki waliopendezwa na mila na destruri za wachina kwenye maudhui.

    Mkurugenzi mkuu wa idhaa ya Radio China Kimataifa ameahidi kwamba Cri na TBC zimepata ufanisi mkubwa katika vipindi vya maendeleo ,uchumi na utamaduni baina ya China Kenya na Tanzania.

    Watanzania 10 watapata fursa ya kufika China kwa ajili ya tafsiri ya tamthilia nyingine za kichina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako