• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Somalia zaahidi kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-03-24 09:14:53

    Marais wa Kenya na Somalia jana waliahidi kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi, kwa kupambana bila huruma na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab, ambao wameongeza mashambulizi ya kigaidi kwenye nchi hizo mbili.

    Rais Uhuru Kenyatta na Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wamekubaliana kuendelea na mapambano dhidi ya kundi la al-Shabaab hadi litakapokuwa sio tishio.

    Akiongea mjini Nairobi kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo na mgeni wake kutoka Somalia, Rais Kenyatta amesema kundi la Al Shabaab bado liko tayari kuua raia wasio na hatia nchini Kenya na Somalia.

    Kwa upande wake Rais Mohamed ameipongeza Kenya kwa mchango wake mkubwa kwenye mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako