• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza kwa hatua madhubuti mchakato wa utandawazi wa dunia nzima

    (GMT+08:00) 2017-03-24 17:45:52

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Zhang Gaoli amesema inapaswa kuhimiza kwa hatua madhubuti mchakato wa utandawazi wa dunia nzima.

    Zhang amesema hayo leo alipoongea na wanaviwanda wa China na nchi za nje katika Mkutano wa mwaka 2017 wa Baraza la Asia la Bo'ao mkoani Hainan, China. Amesisitiza kuwa, mchakato wa utandawazi wa dunia unahitaji maendeleo ya uwezo wa uzalishaji wa jamii na matokeo ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, pia umekuwa msukumo mkubwa katika kuhimiza ongezeko la uchumi duniani, na kutoa fursa nyingi za maendeleo.

    Naye Makamu rais wa Benki ya Maendeleo ya Asia ADB Stephen Groff amesema, uchumi wa China uko imara na muundo wake wa mageuzi uko kwenye mwelekeo mzuri. Akizungumza kwenye mkutano huo, Groff amesema ukuaji wa asilimia 6.7 uliokadiriwa na serikali ya China unaendana na makadirio ya ADB.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako