• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magufuli afanya ziara ya kushtukiza bandarini Dar es salaam

    (GMT+08:00) 2017-03-24 18:27:19

    Rais John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam na kukamata makontena 20 yaliyokuwa yamebeba mchanga wenye madini kutoka migodi iiyopo kanda ya Ziwa pamoja na makontena 10 yaliyokuwa ya magari ya kifahari huku stakabadhi zikionesha kuwa yalikuwa yamebeba mitumba ya nguo na viatu.

    Rais Magufuli alifanya ziara hiyo ya kushtukiza ili kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa ajili ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini humo kupitia bandari hiyo, ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.

    Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa polisi nchini Tanzania Bwana Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo hadi uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako