• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaunti ya Embu Kenya kutumia shilingi bilioni 2.3 kufadhili kilimo biashara katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

    (GMT+08:00) 2017-03-24 18:27:59

    Serikali ya Kaunti ya Embu imesema itatumia shilingi bilioni 2.3 kufadhili kilimo biashara katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Kitita hicho kitatumika katika kupanua miundo mbinu katika mtandao wa kilimo mashambani hadi sokoni; ukarabati wa barabara ukizingatiwa kwa kiwango kikuu ili kurahisisha uchukuzi wakulima na bidhaa zao hadi sokoni. Aidha, serikali hiyo imesema itatafuta mfadhili wa kifedha kutafuta Sh265 milioni za kuzidisha ufadhili wa kilimo biashara. Pia shilingi milioni 100 zitatumika katika sekta ya mboga na matunda huku nyingine 739 zikitumika kukarabati barabara za mashambani.

    Ili kufanikisha ukarabati huo, serikali hiyo itanunua greda nne kwa gharama ya shilingi milioni 100 na kukwepa gharama kubwa ya kukodisha greda kutoka kampuni za kibinafsi. Kitita kama pia hicho kitatumika kuzindua upya sekta ya macadamia ambayo imefifia kufuatia shughuli za mawakala kuwalaghai wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako