• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • PAC yataka mashirika ya umma kuchangia bajeti ya Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-03-24 18:28:23

    Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji Mitaji ya Umma nchini Tanzania (PAC) imeyataka mashirika ya umma 265 nchini humo kujiandaa kuchangia bajeti ya serikali kuanzia mwaka ujao wa fedha.

    Aidha, wakurugenzi na wenyeviti wa bodi wa mashirika hayo kuanzia mwaka ujao watatakiwa kuwasilisha bajeti zao bungeni ili kupitishwa na bunge la Tanzania. PAC imesema hakuna shirika lolote la serikali litakaloweza kupitishwa bajeti bila kuidhinishwa na Bunge.

    Mwenyekiti wa kamati hiyo Bwana Albert Ntabaliba amesema licha ya mashirika hayo kuwa na thamani kubwa ya shilingi trilioni 26, hayajafanikiwa kuchangia ipasavyo bajeti ya serikali, hivyo yanatakiwa yabadilike na kuanza kulipa kodi ipasavyo pamoja na kutoa gawio serikalini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako