• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa vyombo vya habari vya China na nchi za nje wakubaliana kuanzisha Jumuiya ya ushirikiano wa vyombo vya habari ya Asia

    (GMT+08:00) 2017-03-24 20:50:39

    Mkutano wa viongozi wa vyombo vya habari katika Mkutano wa mwaka 2017 wa Baraza la Asia la Bo'ao umefanyika alhamis wiki hii huko Bo'ao, mkoani Hainan.

    Viongozi 21 kutoka nchi 15 zikiwemo China, Marekani, Russia, na Japan, wamejadiliana kuhusu mustakabali wa ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya Asia, na kufikia makubaliano ya kuanzisha Jumuiya ya ushirikiano wa vyombo vya habari vya Asia.

    Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni mkuu wa Radio China Kimataifa Bw. Wang Gengnian alisema, kuongeza kwa hatua halisi uwezo wa uenezi wa kimataifa na sauti za vyombo vya habari vya Asia ni matumaini ya pamoja ya vyombo vya habari vya kanda hiyo. Kufuatia makubaliano hayo, jumuiya ya ushirikiano wa vyombo vya habari, serikali na viwanda inayovuka mipaka ya nchi na kanda itaanzishwa ndani ya siku chache zijazo, na itachangia katika kuwanufaisha wananchi wote wa Asia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako