• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi apongeza kufunguliwa mkutano wa mwaka wa Baraza la Bo'ao

    (GMT+08:00) 2017-03-25 10:17:35
    Mkutano wa mwaka 2017 wa Baraza la Asia la Bo'ao umefunguliwa leo huko Bo'ao, mkoani Hainan, China. Rais Xi Jinping wa China ameuandika barua ya pongezi kuhusu kufunguliwa kwa baraza hilo.

    Rais Xi amesema miaka 16 tangu Baraza la Asia la Bo'ao lianzishwe, baraza hilo limetoa mchango muhimu katika kufikia maoni ya pamoja barani Asia, kuhimiza ushirikiano, na kuongeza ushawishi wa Asia.

    Rais XI amesisitiza kuwa kaulimbiu ya mkutano huo ya "Kukabiliana na utandawazi duniani na mustakabali wa biashara huria", inaonesha ufuatiliaji wa jumuiya ya kimataifa haswa nchi za Asia, juu ya mafungamano ya kiuchumi duniani.

    Pia rais Xi ameeleza matumaini yake kuwa, washiriki watachangia busara zao kwa ajili ya kutatua matatizo makubwa yanayoukabili uchumi wa kikanda na duniani, kuhimiza kwa pamoja mchakato wa utandawazi ulio endelevu, wenye uhai na mapatano zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako