• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Baraza la Asia la Bo'ao kwa mwaka 2017 waanza

    (GMT+08:00) 2017-03-25 19:14:36

    Mkutano wa Baraza la Asia la Bo'ao kwa mwaka wa 2017 umeanza leo mkoani Hainan, kusini mwa China, na rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi akitaka washiriki wa mkutano huo watumie busara zao na kuchangia utatuzi wa masuala makubwa yanayokabili uchumi wa dunia na wa kikanda na kusukuma mbele mchakato wa mafungamano ya kiuchumi ulio hai, jumuishi na endelevu.

    Likiwa shirika la kimataifa lisilo la kiserikali na la kibiashara, Baraza la Asia la Bo'ao ambalo limeanzishwa mwaka 2001 limekuwa likilenga kusukuma mbele ushirikiano wa uchumi wa eneo la Asia na kutoa uungaji mkono kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi ya eneo hilo. Mkutano wake wa mwaka huu wenye kaulimbiu ya "kukabili uso kwa uso siku za baadaye za utandawazi na uhuru wa biashara" unahudhuriwa na wadau wa sekta za siasa, viwanda, biashara na wasomi zaidi ya 1,700 kutoka nchi zaidi ya 50 duniani ambao watajadili mada nne za "Ukanda Mmoja na Njia Moja", "ongezeko", "mageuzi" na uchumi mpya.

    Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo, naibu waziri mkuu wa China Zhang Gaoli amesema maendeleo ya Asia hayapatikani bila dunia, na pia ustawi wa dunia haupatikani bila Asia. Anasema,

    "Nchi za Asia zinashiriki kwenye mchakato wa utandawazi, kutimiza maendeleo ya kasi, kutengeneza miujiza ya Asia, kusukuma mbele ukuaji wa uchumi wa dunia, kutoa fursa za Asia, kupata njia ya kisasa yenye umaalumu wa Asia na kulimbikiza uzoefu wa Asia. Nchi za Asia zinashikilia kukumbatia utandawazi badala ya kuupinga, ambapo sio tu zimepata mafanikio mengi bali pia zimetoa mchango mkubwa kwa ajili ya mafungamano ya uchumi wa dunia."

    Bw. Zhang pia ametoa mwito kwa pande zote kushikilia mtazamo wa kujiendeleza kwa amani, ubunifu, uwazi, kunufaishana na haki, kuimarisha ushirikiano wa kikanda, kujenga uchumi wa dunia wenye ubunifu na kuwa na nia imara ya kusukuma mbele mafungamano ya kiuchumi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako