• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lam Cheng Yuet-ngor achaguliwa kuwa mkuu mpya wa Hong Kong

    (GMT+08:00) 2017-03-26 17:50:18

    Bibi Lam Cheng Yuet-ngor ameshinda kwenye uchaguzi wa afisa mkuu wa tano wa mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong, China.

    Tume ya uchaguzi ya Hong Kong imetangaza kuwa, Bibi Lam amepata kura 777 kati ya 1,163 zilizopigwa, akifuatwa na Tsang Chun-wah aliyepata kura 365 na Woo Kwok-hing kura 21.

    Ofisi ya mawasiliano ya serikali kuu ya China mkoani humo imempongeza Bibi Lam kwa ushindi wake huo na kumtarajia kuongoza serikali ya Hong Kong kuunganisha sekta mbalimbali za jamii, kutekeleza sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" na Sheria ya Msingi ya Hong Kong kwa ukamilifu na usahihi, kujitahidi kuendeleza uchumi, kuboresha maisha ya watu na kuhimiza utulivu na masikilizano kwenye jamii.

    Wakati huohuo, Ofisi ya mambo ya Hong Kong na Macao ya Baraza la Serikali la China imesema, uchaguzi huo ulifanyika kwa haki na Bibi Lam amekidhi vigezo vilivyowekwa

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako