• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) yaibamiza Timu ya Taifa ya Botswana

    (GMT+08:00) 2017-03-27 08:22:54

    Mabao 2 yaliyofungwa na nahodha Mbwana Ally Samatta yametosha kuipa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa jumamosi uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Huo ulikuwa mchezo wa kwanza Taifa Stars inacheza chini ya kocha wake mpya, Salum Mayanga aliyerithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa aliyeng'atuka mwezi Janauri.

    ilimchukua dakika 2 tu mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji kuwainua vitini wapenzi wa soka wa Tanzania waliojitokeza Uwanja wa Taifa baada ya kupokea pasi ya winga Shiza Kichuya na kumtoka beki Kaone Vander westhuizem kabla ya kumchambua kipa, Kabelo Dambe.

    Samatta aliongeza bao la 2 katika dakika ya 87 ya mchezo baada ya kupokea pasi safi toka kwa Farid Mussa anayechezea timu ya Tenerife ya Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako