• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu ya Raga nchini Kenya: Mean Machine yaaga

    (GMT+08:00) 2017-03-27 08:23:27

    Mean Machine imeaga ligi kuu ya Raga ya Kenya baada ya kupigwa 21-12 na Nakuru, Jumamosi.

    Mchuano huo ulikuwa wa mwisho wa timu hiyo ya Chuo Kikuu cha Nairobi katika msimu wa kawaida wa ligi hiyo ya klabu 12.

    Machine imemaliza ikishikilia mkia kwa pointi 11 baada ya kushinda mechi 2 na kupoteza 14.

    Klabu hiyo, ambayo ilianzishwa mwaka 1977, imekuwa ikifanya vibaya miaka ya hivi karibuni na hata kuponea chupuchupu kutemwa 2014-2015 na 2015-2016 ilipomaliza nafasi moja juu ya mduara hatari wa kutemwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako