• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuelekea Kombe la Dunia 2018 Russia: Ubelgiji yaponyeka, wadachi hoi, Ronaldo aibeba Ureno

    (GMT+08:00) 2017-03-27 08:24:37

    Mechi za makundi ya Ulaya kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia zimeendelea Jana kwa Ubelgiji kunusurika kipigo toka kwa Ugiriki baada ya kulazimishwa sare ya 2-2. Ugiriki walitangulia kufunga dakika ya 46 kwa bao la Kostas Mitroglou na dakika ya 65 huku Ubelgiji wakijipatia magoli yake kupitia kwa Lukaku.

    Wakicheza kwao Estadio da Luz, Ureno waliishinda Hungary 3-0 na kubaki nafasi ya Pili kwenye Kundi B wakiwa Pointi 3 nyuma ya Switzerland ambao nao waliifunga Latvia 1-0.

    Bao za Ureno zilifungwa dakika za 32, 36 na 65 kupitia Andre Silva na 2 za Ronaldo.

    Na huko Sofia, Bulgaria waliichapa Netherlands 2-0 na kuwaweka hatarini kutofuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia.

    Bao za Bulgaria zilifungwa na Spas Delev katika Dakika za 5 na 20.

    Matokeo katika kundi A, Ufaransa imeicharaza Luxembourd goli 3-1.

    Katika kundi C, Uingereza imeifunga Lithuana 2-0, Jamhuri ya Czech ikiibamiza San Marino 6-0, Ujerumani imeifunga Azerbaijan 4-1. Huku katika kundi F, Uingereza imeifunga Lithuania 2-0.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako