• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madaktari wa China wagawa upendo kwa wakaazi wa Kibera Nairobi

    (GMT+08:00) 2017-03-27 19:01:00

    Bwana Lei Wang ni daktari wa China anayetoa huduma nchini Kenya.

    Yeye na madaktari wengine ambao wametuma nchini Kenya kutoa msaada wa matibabu wamekuwa wakitoa huduma kwenye jamii masikini hasa kwa watoto na wazee.

    Lakini pia mbali na huduma za matibabu Daktari Wang na wenzake hivi karibuni alizuru mtaa wa Kibera mjini Nairobi ambao ni mojawepo wa mitaa ya watu wenye mapato ya Chini na kutoa zawadi kwa wakaazi.

    Baadhi ya zawadi walizotoa pipi, sashi (wet wipes) na sabuni.

    Msaada huo umetolewa chini ya mkakati wa Sino Africa Firefly Charity ulioanzishwa hivi karibuni na daktari Leo Wang.

    Ikiwa na jina Sino Africa Firefly Charity, msaada huu wa kibera ni maalum na wa aina yake kwa wakaazi wa Kibera.

    Daktari Lei Wang anawaalika wachina kutembelea moja kwa moja wakaazi wa hapa na kutoa misaada wao wenyewe.

    Kwa kufanya hivyo wanaweza kujumuika na wenyeji na pia kujionea hali ya maisha yao ya kila siku huku wakitoa mchango wao kama sehemu ya wajibu wa wachina kwa jamii nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako