• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar:ya ahidi kuboresha mazingira ya uwekezaji

    (GMT+08:00) 2017-03-27 19:43:54

    SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wadau wengi zaidi kuwekeza humo hasa katika mji wa Pemba.

    Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada alisema hayo katika hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi wa 4G pamoja na huduma za kibenki kwa njia ya simu kutoka kampuni ya Zantel.

    Alisema serikali itaendelea kuhakikisha huduma za kifedha kwa pamoja na mawasiliano zinawafikia Wazanzibari wote kwa urahisi .

    Alisema katika kuhakikisha hilo linafanyika Serikali ya Zanzibar imeendelea kufanya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu hasa barabara, njia za mawasiliano na utengenezaji wa sera zilizo stahiki pamoja na kupigana na umasikini na ukosefu wa elimu kwa wananchi wa Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako