• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za nyika za Dunia: Kenya yazoa medali 12

    (GMT+08:00) 2017-03-28 08:51:33

    Kenya imeshinda mbio za nyika za Dunia za mwaka 2017 baada ya kuzoa medali 4 za dhahabu, 5 za fedha na 3 za shaba uwanjani Kololo jijini Kampala nchini Uganda, Jumapili.

    Geoffrey Kamworor na Irene Cheptai waling'aa katika vitengo vya watu wazima naye Asbel Kiprop akaongoza Wakenya kushinda kitengo kipya cha mbio za kupokezana vijiti.

    Kenya pia ilinyakua mataji ya timu ya vitengo vya watu wazima na kupokezana vijiti.

    Mahasimu wakuu wa Kenya, Ethiopia walimaliza mashindano hayo ya siku moja katika nafasi ya 2 kwa kuzoa dhahabu 4, fedha 4 na shaba 1, nao wenyeji Uganda wakafunga tatu-bora kwa kuvuna dhahabu 1 na shaba 2.

    Uturuki, Eritrea na Bahrain walishinda nishani 1 ya shaba kila mmoja, huku Tanzania ikiambulia patupu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako