• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya Prisons kuchuana na FAP ya Cameroon

    (GMT+08:00) 2017-03-28 08:52:43

    Mabingwa wa Taifa wa mpira wa wavu, Kenya Prisons watachuana na timu ya FAP ya Cameroon kwenye mechi ya uorodheshwaji ya michuano inayoendelea ya Bara Afrika baina ya vilabu vya wanaume, baada ya kushindwa na vigogo Al Ahly ya Misri seti kwa sifuri kwenye robo fainali jijini Tunis, Tunisia. "Kenya Prisons" ilimaliza ya pili katika kundi 'D' nyuma ya wenyeji Sahel na kufuzu kwa robo fainali lakini wakashindwa kukabiliana na timu hiyo kutoka Afrika Kaskazini. Timu hiyo ya Kenya ilipoteza kwa seti za 25-15, 25-13 na 25-19 na kutolewa kwenye mashindano ya mwaka huu. Kwenye mechi nyingine ya robo fainali, Etoile Du Sahel ya Tunisia iliwashinda wenzao Esperance seti tatu kwa mbili na kufuzu kwa nusu fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako