• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsenal watupwa nje Kombe la FA

    (GMT+08:00) 2017-03-28 08:53:21

    Mabingwa watetezi wa kombe la FA la wanawake nchini Uingereza, kina dada wa Arsenal wametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kuchapwa 1-0 na kina dada wa Birmingham City katika hatua ya robofainali.

    Bao la Birmingham lilifungwa na Marisa Ewers dakika ya 77. Huku kipa wa Birmingham Ann-Katrin Berger alifanya kazi ya ziada kuwazuia Arsenal kufunga. Aliokoa makombora kutoka kwa Kim Little, Danielle Carter na Danielle van de Donk kipindi cha kwanza.

    Katie McCabe na Jordan Nobbs walishambulia lakini wakashindwa kulenga vyema wavu upande wa Arsenal muda mfupi kabla ya Ewers kufunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako