• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kufuzu kombe la Dunia 2018: leo Jumanne, Marekani kusini kugombea nafasi, je Brazil yenyewe itafanikiwa kufuzu?

    (GMT+08:00) 2017-03-28 08:54:04

    Mechi kwa ajili ya kufuzu kuingia katika michuano ya kombe la Dunia mwakani nchini Russia zinaendelea leo Jumanne. Mechi ambayo inatarajiwa kuwa na mvutano mkubwa ni ile ya Ecuador na Colombia ambayo kila mmoja anataka kumng'oa mwenzake kwenye nafasi ya 4 ambayo ndiyo ya mwisho kufuzu moja kwa moja kwenda Fainali Russia.

    Mechi hii ambayo itachezwa nyumbani kwa Ecuador huko Estadio Olimpico Atahualpa, Mjini Quito, ni wazi inaipa faida kubwa Ecuador kwakuwa watakuwa nyumbani.

    Kwingineko mjini Lima, Peru watakuwa wenyeji wa Uruguay ambao Juzi walitandikwa 4-1 na Brazil huko kwao Montevideo lakini wana kibarua kigumu kuifunga Uruguay ambayo wamewahi kuifunga mara 1 tu kwenye Mechi za Kombe la Dunia.

    Nao Bolivia, wataikaribisha Argentina ambao watawakosa wachezaji wao Javier Mascherano na Gonzalo Higuain ambao wamefungiwa na kuwa na majeruhi. .

    Chile, wako nyumbani kucheza na timu ya mkiani Venezuela huku wakitegemea ushindi laini hasa baada ya Staa wao Arturo Vidal kurejea Kikosini.

    Nao vinara Brazil, ambao watakuwa nyumbani kucheza na Paraguay, Paraguay hawajawahi kuifunga Brazil huko kwao na mara ya mwisho kuambua Pointi 1 ni Mwaka 1985.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako