• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuipatia Zimbabwe msaada wa dola milioni moja kupambana na mafuriko

    (GMT+08:00) 2017-03-28 09:53:09

    Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw Huang Ping amesema China itaipatia Zimbabwe msaada wa dola milioni moja za kimarekani ili kuwasaidia wananchi wanaokabiliwa na maafa ya mafuriko nchini humo.

    Amesema mwaka huu serikali ya China itatoa msaada wa dola milioni moja za kimarekani kwa ajili ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko nchini Zimbabwe. Kamati ya msalaba mwekundu ya China pia itatoa msaada wa dola elfu hamsini za kimarekani. Zaidi ya hayo, ubalozi wa China na jumuiya ya wachina zitachangia Zimbabwe dola elfu kumi.

    Mvua kubwa nchini Zimbabwe iliyotokana na kimbunga cha Dineo imesababisha vifo vya watu 271, na wengine 128 kujeruhiwa, na wapatao elfu mbili kupoteza makazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako