• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenzake wa Madagascar

    (GMT+08:00) 2017-03-28 18:06:30

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na mwenzake wa Madagascar Bw. Hery Rajaonarimampianina.

    Rais Xi amesema, katika miaka 45 iliyopita tangu China na Madagascar zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizo mbili zinaheshimiana, kuelewana na kuungana mkono katika masuala yanayohusu maslahi na ufuatiliaji wao mkuu. China inakaribisha Madagascar kushiriki kwenye ujenzi wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kuiunga mkono nchi hiyo iwe daraja la kuunganisha pendekezo hilo na Afrika. Rais Xi ameongeza kuwa, China inaiunga mkono Madagascar kufanya kazi kubwa zaidi katika mambo ya kimataifa na kikanda, na inapenda kuimarisha mawasiliano zaidi kati ya pande hizo mbili katika mabadiliko ya hali ya hewa, ajenda ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu ya mwaka 2030 na maswala mengineyo.

    Rais Hery amesema, nchi yake inapenda kuimarisha ushirikiano kati yake na China, ili kuchangia maendeleo ya uchumi na jamii nchini mwake, na kuhimiza mchakato wa viwanda nchini Madagascar na barani Afrika. Vilevile nchi yake inaunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kutumai kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za nishati, safari za anga, mawasiliano barabarani, ujenzi wa bandari na uwanja wa ndege.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako